Lyrics: UJULIKANE – Karwirwa Laura ft Alice Kimanzi

Lyrics: UJULIKANE – Karwirwa Laura ft Alice Kimanzi

Nisijione mkamilifu, kwa nguvu zangu
Nitaweza pekee yangu
Nisiamini hekima yangu
Juhudi zangu, nikutazamie Mungu
Watakao nisikia wakinishangilia,
Niwaelekeze kwako ooh
Watakaonifuata nikikufuata, tuje kwako
Na chochote kile itaenda sawa
Sio mimi wewe ujulikane
Na popote pale nitaenda baba
Sio mimi wewe ujulikane .

Ujulikane ujulikane
Ewe Yesu ujulikane
Ujulikane ujulikane
Ewe Yesu ujulikaneKwa maneno yangu tena matendo yangu
Natamani wewe ujulikane
Kama vile maji ifunikavyo bahari
Natamani wewe ujulikane
Uokoe waliofungwa,uponye waliozidiwa
Uinue waliolemewa aah
Hakuna usichokiweza Baba aah

Chochote kile kitaenda sawa
Sio mimi wewe ujulikane
Na popote pale nitaenda baba
Sio mimi wewe ujulikane .

Ujulikane ujulikane
Ewe Yesu ujulikane
Ujulikane ujulikane
Ewe Yesu ujulikane

Uokoe waliofungwa,aah
Uponye waliozidiwa,aah
Uinue waliolemewa aah
Baba ujulikane

Ujulikane ujulikane
Ewe Yesu ujulikane
Ujulikane ujulikane
Ewe Yesu ujulikane

Read more: UJULIKANE video release

Phoenix

Phoenix is the founder of Let Music Preach. He is also a creative who writes, deejays, does digital design and photography. He is passionate about using music to influence the masses.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

%d bloggers like this: